Exodus 39:8-13

8 aAkafanyiza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. 9Kifuko hicho kilikuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja
Shibiri moja ni sawa na sentimita 22.
na upana wa shibiri moja, nacho kilikunjwa mara mbili.
10 cKifuko hicho kilipambwa kwa safu nne za vito vya thamani. Safu ya kwanza ilikuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 11 dsafu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 12safu ya tatu ilikuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 13 ekatika safu ya nne ilikuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Vito hivyo vilitiwa kwenye vijalizo vya dhahabu.
Copyright information for SwhKC